Rais Samia Suluhu Hassan amemuapisha Balozi Yusuf Mndolwa kuwa Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol) katika wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Hafla ya kumuapisha Balozi Mndolwa imefanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Balozi Mndolwa anachukua nafasi iliyoachwa na Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Baada ya kiapo hicho Balozi Mndolwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Benedict Ndomba wamekula kiapo cha maadili kwa viongozi wa umma kilichosomwa na Kamishna wa Maadili ambaye pia ni Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufani Sivangilwa Mwangesi.

Kabla ya uteuzi huo Ndomba alikuwa Mkurugenzi wa Miundombinu na Operesheni wa eGA na anachukua nafasi ya Dkt. Jabir Kuwe ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).