Rais Samia Suluhu Hassan leo ameshiriki Hitima ya kumbukumbu ya miaka 49 ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume, iliyofanyika katika ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mkoa wa mjini Magharibi.

Hitma ya Hayati Karume imesomwa na Sheikh Mohamed Abbas ambapo viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla.

Katika mawaidha yake baada ya Kisomo hicho, Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Zanzibar Sheikh Shabaan Salum Bapashi amemuelezea Hayati Karume kuwa alikuwa ni kiongozi aliyewapenda watu wake na ndio maana aliwafanyia maendeleo makubwa.

Sheikh Bapashi amesema kuwa Watanzania wanapaswa kuwaenzi viongozi wote waliotangulia mbele ya haki na kuyaenzi yale yote waliyoyafanya.

Aidha ametoa Pole kwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa misiba iliyolipata Taifa katika kipindi kifupi