Ikiwa leo April 4, 2021 Wakristo wa Tanzania wanaungana na wenzao duniani kuadhimisha sikukuu ya Pasaka ambayo KikrIsto ni maadhimisho ya kuteswa kufa na kufufuka kwa mwokozi wao yaani Yesu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewatakia heri.

Salamu hizo za Pasaka amezitoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ambapo amewaasa kuendelea kuliombea taifa kudumisha upendo, amani na mashikamano.
 

"Nawatakia watanzania wote Pasaka njema, tuadhimishe ufufuko wa Yesu Kristo huku tukiliombea Taifa letu la Tanzania kudumisha amani, upendo na mshikamano. Tuendeleze jitihada za kuijenga nchi yetu kwa kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa.Yesu amefufuka, Haleluya Haleluya."

Pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi amewatakia Pasaka njema wakristo wote.

"Nawatakia Wazanzibari wote na Watanzania kwa ujumla heri ya sikukuu ya Pasaka. Tuendelee kudumisha na kuthamini amani ya nchi yetu."