Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kushughulikia sakata la kupanda kwa gharama za vifurushi vya simu lililoibuka kuanzia Aprili 2, 2021.

Rais Samia  ameeleza hayo leo Jumanne Aprili 6, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaapisha makatibu wakuu na manaibu wao aliowateua Aprili 4, 2021.

 “Kulizuka rapsha rapsha juzi hapa kuhusu masuala ya mabando wananchi wakawa juu mkalituliza. Kalifanyieni kazi lisizuke namna ile, mpo na mnaangalia. Hawa watu wanakuja na mambo yao wananchi wanashtuka ndiyo na nyie mnashtuka, hapana,” amesema Rais Samia.


Kuhusu mkongo wa Taifa, Rais Samia amesema kuna haja na kuwa na tamko la kisera kuhusu mkongo huo na sio wenye mitandao ya simu kuanzisha mikongo yao, jambo ambalo si salama kwa nchi.