Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Juma Selemani Mkomi kuwa Katibu wa Rais (KR).

Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Machi, 2021.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Samia amefanya uteuzi wa Wasaidizi katika Ofisi Binafsi ya Rais (OBR) kama ifuatavyo;

  1.  Amemteua Bw. Said Ali Juma kuwa Mnikulu.
  2.  Amemteua Mhe. Balozi Dkt. Mussa Julius Lulandala kuwa Msaidizi wa Rais, Nyaraka na Ukalimani (PAP-TD).
  3.  Amemteua Mhe. Balozi Ali Bujiku Sakila kuwa Msaidizi wa Rais, Hotuba (PAP-SD).
  4.  Amemteua Bi. Maulidah Bwanaheri Hassan kuwa Msaidizi wa Rais, Diplomasia (PAP-DA).
  5. Amemteua Bi. Felister Peter Mdemu kuwa Msaidizi wa Rais, Maendeleo ya Jamii.
  6.  Amemteua Bw. Nehemia Ernest Mandia kuwa Msaidizi wa Rais, Sheria (PAP-LA)
  7. Amemteua Dkt. Blandina Kilama kuwa Msaidizi wa Rais, Uchumi (PAP-EA).
  8. Amemteua Dkt. Salim Othman kuwa Msaidizi wa Rais, Siasa (PAP-PA).