Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Manyara, inamshikilia Mwendesha Mashtaka wa Serikali mkoani humo Wakili Mutalemwa Kishenyi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni tano.

Wakili Kishenyi alikamatwa na Maafisa wa TAKUKURU tarehe 23 mwezi huu akiwa amepokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa watuhumiwa wa makosa ya jinai.

Watuhumiwa hao wa makosa ya jinai walikamatwa hivi karibuni kufuatia upekuzi uliofanywa na vyombo vya dola ambapo walikutwa na vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na risasi 370.

Katika hatua nyingine TAKUKURU mkoa wa Manyara imemtaka mkurugenzi wa kampuni ya Mati Super Brands David Mulokozi kufika katika ofisi za TAKUKURU baada ya kukaidi wito aliopewa kwa madai kuwa ana shughuli za biashara.

TAKUKURU imesema kukaidi wito ni kosa kisheria.