Mwanamfalme Philip, mume wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99.

Tangazo kutoka Kasri ya Buckingham linaeleza: "Ni kwa masikitiko makubwa, Malkia ametangaza kifo cha mumewe mpenzi, Mwanamfalme Philip, Duke (Mtawala) wa Edinburgh."

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anasema ni "kwa huzuni kubwa" kupokea habari za kifo cha Mwanamfalme Philip kutoka Kasri la Buckingham.

Mwanamfalme Philip alimuoa Bintimfalme Elizabeth mnamo 1947, miaka mitano kabla ya kuwa Malkia, na amekuwa mwenza wa mfalme ama malkia aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza.