Urusi na Marekani zinaripotiwa kuwa na mawasiliano ya ngazi za juu kuhusiano na hali ya Ukraine. 

Shirika la habari la Urusi, Interfax, limemnukuu Naibu Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi, Sergei Ryabkov, akisema kwamba pande hizo mbili zimekuwa na mazungumzo ya pamoja. 

Kwa mujibu wa waziri huyo, Urusi imeifahamisha Marekani kwamba hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi, licha ya kuwapo harakati za kijeshi karibu wa mpaka wake na Ukraine. 

Ryabkov amesema hakuna uwezekano wa kuzuka kwa mapigano baina ya pande hizo mbili, kwani kuwepo kwa jeshi lake kwenye eneo hilo si kitisho kwa Ukraine wala kwa nchi nyengine. 

Hivi karibuni, Ikulu ya White House ilisema kuwa inatiwa mashaka na taarifa za Urusi kutuma wanajeshi wake kwenye mpaka wake na Ukraine, huku ikiashiria utayarifu wa Marekani kuingilia kati kwa maslahi ya Ukraine.