Mbunge wa Vunjo, Dk Charles Kimei amesema deni la taifa ni himilivu na thamani ya shilingi ni nzuri na Serikali inaweza kutumia kwenda kukopa fedha kwenye soko la dunia kwa riba ndogo ili kukamilisha miradi mikubwa nchini.

Kimei ametoa kauli hiyo bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha mpango wa tatu wa maendeleo ya kitaifa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021/22 – 2025/26.

Amesema  hakuna sababu ya kucheleweshwa kwa ujenzi wa miradi mikubwa ya mkakati  ikiwemo reli ya kisasa SGR na   bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere ambayo ni chachu kwa ukuaji wa uchumi wanchi

 “Hakuna sababu ya kuchelewesha  wa utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa kama SGR na mradi wa umeme wa Mwalimu Nyerere wakati tunaweza kukopa na kukamilisha haraka na kuona matunda kwa miradi hiyo mikubwa ambayo ni chachu katika ukuaji wa taifa letu,”amesema


Pia ameipongeza Serikali kwa kuuweka uchumi wa nchi kwenye hali ya utulivu na nzuri katika kipindi cha ugonjwa wa Covid-19 na mfumuko wa bei uko chini.