Kila staa ana role model wake ambaye siku akifariki basi hutaka kukumbukwa ama watu wamuenzi kama yeye ikiwa ni ishara ya kwamba mtu huyo mashuhuri ameacha alama katika ulimwengu huu ambao hauwezi kusahaulika katika taswira za watu

Tumewahi kuona baadhi ya mastaa kama Lil Wayne yeye aliwahi kuimba katika moja ya ngoma yake kuwa siku akifariki anahitaji akumbukwe kama marehemu 
John Lenon

"If i die today remember me like 
John LenonLil Wayne ft Rick Ross John

Hivi karibuni Rapa 
Jay Z naye akiwa kwenye mahojiano na The Sunday Times ameripotiwa akisema kuwa siku akifariki basi watu wamkumbuke kama marehemu Bob Marley akiwa kama mtu mashuhuri aliyeacha alama ulimwenguni

"Sina majivuni, si ndio ? Natumai wataniongelea Mimi pamoja na majina kama Bob Marley na wengine wakubwa. Mimi sipo kwenye upande wa kuizungumzia." alisema Jay-Z alipoulizwa kuhusu watu wamkumbuke vipi, kwenye mahojiano na The Sunday Times.