Afisa mkuu katika kituo cha kudhibiti magonjwa China amekiri kwamba chanjo iliyotengenezwa nchini humo ni hafifu katika kuzuia maambukizi ya virusi vya corona. 

Akizungumza katika mkutano jana, Gao Fu ambaye ni mkurugenzi katika shirika hilo amesema serikali ya China inatafakari kuchanganya chanjo tofauti ili kuongezea nguvu chanjo hiyo. 

Katika mkutano na waandishi wa habari, maafisa wa shirika hilo hawakujibu moja kwa moja maswali kuhusiana na matamshi ya Gao huku mkurugenzi huyo akiripotiwa kutojibu simu kwa ajili ya kuzungumzia zaidi hayo aliyoyasema. 

China imesambaza mamilioni ya dozi za chanjo katika nchi za nje huku ikiendesha kampeni ya kuiponda chanjo ya Pfizer-BioNTech.