Mkutano mkuu maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaofanyika jijini Dodoma, umemchagua Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa.

Rais Samia Suluhu Hassan anakuwa Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Rais Samia Suluhu Hassan amepata kura zote 1, 862 zilizopigwa na Wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM, ikiwa ni ushindi wa asilimia mia moja.