Kiongozi wa upinzani nchini Urusi aliye gerezani Alexei Navalny ametangaza kusitisha mgomo wa kula baada ya kupatiwa msaada wa matatibu na kuonywa na madakatari kuwa kususia chakula kunatishia uhai wake.

Katika ujumbe alioutoa kupitia ukurasa wake wa Instargam siku ya 24 tangu kuanza kwa mgomo huo, Navalny amesema anasitisha uamuzi wake wa kukataa chakula baada ya kufanikiwa kuonana na madaktari huru waliochunguza afya yake.

Kupitia ujumbe huo Navalny amewashukuru wafuasi wake kwa kumuunga mkono na amesisisitza licha ya kusitisha mgomo bado ataendelea kushinikiza matakwa yake ikiwemo haki ya kutembelewa na daktari akiwa jela.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 44 ambaye alikamatwa mapema mwaka huu na anatumikia kifungo cha miaka miwili na nusu jela alianza mgomo wa chakula Machi 31 kupinga maafisa wa magereza kumzuia kukutana na madaktari wake binafsi.