Maafisa wa Afghanistan wameshtumu mpango wa kuondolewa bila masharti wanajeshi wa Marekani nchini humo, mpango ambao unatarajiwa kutangazwa rasmi na Rais Joe Biden baadaye hii leo na kuhitimisha miongo kadhaa ya oparesheni za jeshi la Marekani nchini Afghanistan.

Mpatanishi wa amani wa serikali ya Afghanistan aliyeko mjini Doha na ambaye hakutaka jina lake kutajwa, ameliambia shirika la habari la dpa kuwa uamuzi huo haufai na kwamba ni wa kibinafsi.

Mpatanishi huyo wa serikali amesema huenda ukawa mwisho wa vita kwa Marekani, japo washirika wake ndio huenda wakaathirika zaidi na uamuzi huo.

Naye mkuu wa zamani wa tume huru ya haki za binadamu ya Afghanistan, Sima Samar, pia amesikitishwa na uamuzi huo akiutaja kuwa "bahati mbaya".Marekani iliivamia Afghanistan kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 na kuupindua utawala wa kundi la Taliban.

CREDIT:DW