Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu amesitisha safari yake ya kihistoria kwenda Falme za Kiarabu (UAE) hapo jana baada ya kutokea mzozo na Serikali ya Jordan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya kiongozi huyo imeabainisha kuwa Jordan imezuia anga lake kutumika hivyo Netanyahu alishindwa kufanya safari yake UAE .

Hiyo ingekuwa ziara ya kwanza ya Nentanyahu tangu uhusiano wa kidiplomasia uanzishwe baina ya nchi hizo mbili mwezi Agosti mwaka jana.