Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kushikamana na kuungana, wakati huu ambapo Taifa linapambana na magonjwa mbalimbali na kuacha kusikiliza taarifa za uzushi zinazotolewa na baadhi ya watu.

Makamu wa Rais ametoa rai hiyo wakati akizungumza na Wanachi waliojitokeza kumpokea kwenye mji mdogo wa Makata wilayani Handeni, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku sita mkoani Tanga.

Amewataka Watanzania kushikamana na kuachana na taarifa za uzushi zinayotolewa na baadhi ya watu wasiolitakia mema Taifa, na badala yake waendelee kujenga umoja wa Kitaifa.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pia amewataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi na kuwahakikishia kuwa Taifa liko imara na salama.

Makamu wa Rais ameanza ziara ya siku sita mkoani Tanga, ambapo tayari amezindua jengo la ofisi za halmashauri ya wilaya ya Handeni katika eneo la Makata.