Wizara ya mambo ya nje ya Urusi jana jioni imesema kuwa vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani ni ishara ya wazi ya uhasama dhidi ya nchi hiyo na kusema italipiza kisasi katika kile ilichokitaja kuwa pigo lingine katika ushirikiano kati ya Marekani na Urusi. 

Katika hatua iliyoonekana kama changomoto ya moja kwa moja ya Rais Joe Biden kwa Ikulu ya Urusi, Kremlin, hapo jana Marekani iliweka vikwazo kuiadhibu Urusi katika kile ilichokitaja kuwa juhudi za nchi hiyo za kutaka kumpa sumu mwanasiasa wa upinzani Alexei Navalny mwaka jana. 

Katika kujibu kuhusu hatua hiyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov amesema kuwa watajibu bila kushindwa na kwamba kulipiza ambayo ni moja ya sheria ya kidiplomasia bado hakujafutiliwa mbali. 

Katika taarifa, msemaji wa wizara hiyo ya mambo ya nje Maria Zakharova, amesema kuwa hiki ni kisingizio tu cha Marekani kuendelea kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.

-DW