Umoja wa Mataifa unaonya kuwa jeshi la Myanmar linashiriki kwenye uhalifu dhidi ya binadamu, baada ya watalaam wake kuripoti kuwa watu zaidi ya 70 wameuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama.

Wafuasi wa kiongozi wa kiraia Aung San Suu Kyi, wamekuwa wakiandamana tangu Februari 1, wakishinikiza kuachiliwa kwa kiongozi wao.

Kumekuwa na shinikizo za kidiplomasia kuwataka wakuu wa jehsi nchini humo kuacha kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji.

Waandamanaji zaidi ya 2,000 wanaoshinikiza kuachiliwa huru kwa Suu Kyi, wamekamatwa tangu mwezi Februari.

Jeshi limekuwa likisema chama cha Suu Kyi, cha NLD kiliiba kura wakati wa uchaguzi wa wabunge mwezi Novemba mwaka 2020.

-RFI