Wapiga kura katika majimbo ya Baden Wuerttemberg na Rhineland-Palatinate kusini mashariki mwa Ujerumani wanapiga kura siku ya jana katika uchaguzi wa majimbo utakaosaidia kuamua kuhusu mrithi wa Kansela Angela Merkel baadaye mwaka huu. 

Kura ya maoni ya hivi karibuni inaonesha chama cha kihafidhina cha Christian Democtrat, CDU kikiwa nyuma mno dhidi ya chama cha watetezi wa mazingira cha Green katika jimbo la Baden-Wuerttemberg. 

Chama cha mrengo wa wastani unaogemea kushoto cha Social Democrat SPD; kimekuwa kikijiimarisha katika jimbo la Rhineland-Palatinate na kuongeza matarajio ya waziri mkuu wa jimbo hilo mwenye umaarufu mkubwa Mali Dreyer, kurejea madarakani kama kiongozi wa muungano wa vyama vitatu.