Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
TUME ya Haki za Binadamu na utawala bora nchini imekutana  na wadau  wa Idara,Taasisi na Wizara mbalimbali za Serikali Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili taarifa ya mapendekezo  zaidi ya  227  yaliyotolewa na Baraza la haki za Binadamu Duniani kuhusiana na maendeleo ya masuala ya haki za binadamu.

Akizungumza katika kikao cha kujadili taarifa hiyo,Mwenyekiti wa Tume hiyo,Jaji mstaafu Mathew Mwaimu amesema kuwa Tanzania kama nchi mwanachama wa Baraza hilo la haki za binadamu hutakiwa kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa kama ushauri  kuhusiana na masuala ya maendeleo ya haki za binadamu.

Jaji Mwaimu amesema kuwa kutokana na mapendekezo hayo  ambayo yapo 227 yaliyotolewa na Baraza hilo la haki za binadamu  kwa  Tanzania kama mwanachama ambayo iliyakataa baadhi ya mapendekezo takribani 93 yalitolewa na Baraza hilo mwaka 2016.

 Amesema kila baada ya miaka minne wamekuwa wakituma taarifa ya maendeleo ya haki za binadamu ambapo ifikapo Machi25 mwaka huu Tanzania itapeleka taarifa hiyo makao makuu ya Baraza la haki za binadamu nchini Geneva Uswiss.

 Amesema maeneneo mengine ambayo hawajayaweka katika taarifa hiyo ambayo ina kurasa tano watachagua yale ya muhimu na kupokea ushauri na kuyaboresha mapendekezo hayo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo,Muhamed Hamisi Hamad amesema kuwa taarifa hiyo ya haki za binadamu inahusu Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na wamechukua hatua mbalimbali zimefanyika ikiwemo haki za wanawake ikiwemo uteuzi wa nafasi za wanawake katika uongozi

 Naye Kamishina paul Masanja wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora amesema kuwa Tanzania kama mwanachama wa umoja wa mataifa na wadau wa haki za binadamu wanawajibika kutoa ripoti kwa Baraza hilo ili kuonyesha kama hayo yanafanyika nchini

Kuna masuala mbalimbali ya haki za kijamii na kiuchumi zimefikiwa ikiwemo maji,afya kwa makundi mbalimbali ambapo utekelezaji wake umepiga hatua.