Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ,TAKUKURU,imeaswa kuongeza Juhudi zaidi katika mapambano dhidi ya rushwa ya ngono nchini.

Hayo yamebainishwa leo Machi,2,2021 jijini   Dodoma na Naibu Waziri wan chi,Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora,Deogratius Ndejembi wakati akifungua mkutano ,mkuu wa mwaka wa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na  kupambana  na  rushwa nchini [TAKUKURU].

Naibu Waziri Ndejembi amesema pamekuwa na changamoto ya rushwa ya ngono hususan  kesi zinazopelekwa mahakamani kufutika juu ya mwanafunzi anapopewa ujauzito  hilo ni kutokana na wazazi kutoka pande mbili kuelewana   ,kufanya hivyo ni kosa la rushwa ya ngono na ubakaji  na ni wajibu kwa kesi zote kuendelea  .

Naibu Waziri Ndejembi ametumia fursa kuipongeza TAKUKURU kwa kuleta mafanikio  na  heshima  kubwa katika Taifa la Tanzania

Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo amesema katika taarifa ya utendaji kazi ya TAKUKURU katika kipindi cha Mwezi Julai , 2019hadi  hadi Juni,2020  utekelezaji wa malengo ya uzuiaji rushwa  ulifikia asilimia 89.8% sawa na asilimia 90%.

Aidha,Brigedia Jenerali Mbungo amesema TAKUKURU inazingatia miongozo ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa  sheria Na.11 ya mwaka 2017,mpango mkakati wa TAKUKURU 2017-2022.

Akitoa neno la shukrani kwa Mgeni rasmi,mkurugenzi wa uzuiaji rushwa TAKUKURU,Sabina Senja amekabidhi zawadi kwa Naibu waziri Ndejembi ikiwa ni pamoja na kitabu cha sheria ya kuzuia rushwa ya mwaka 2017, mkakati wa kitaifa wa kuzuia rushwa  awamu ya tatu,Mpango mkakati wa TAKUKURU miaka mitano,mwongozo wa kupambana na rushwa katika taasisi zote  pamoja na taarifa ya utafiti wa rushwa ya ngono wa mwaka 2020.

MWISHO.