Ajali ya moto.
Tarehe 09.03.2021 majira ya saa 15:00hrs huko kambi ya uvuvi Migongo, kata ya Maisome, wilaya ya Sengerema. Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Mussa Adward, Msukuma, miaka 37, mkazi wa mtaa wa Misheni aliyekuwa anafanya kazi ya kubeba mizigo (kuli) mkazi wa Maisome, alifariki dunia baada ya kuungua moto wakati akiingiza pipa lililokuwa na mafuta ya petroli ndani ya kibanda cha kuuzia mafuta. Inadaiwa pipa lilipasuka na petroli kutiririka mpaka kwenye kibanda kilichokuwa na moto ambacho hutumika kuchomea viazi (chips) na kusababisha moto kuwaka na kusambaa sehemu kubwa.
Hata hivyo, jitihada zilizofanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi zilifanikiwa kuuzima moto huo.
Inadaiwa chanzo cha moto huo ni kuvuja kwa petroli iliyokuwa kwenye pipa lililotoboka wakati wa kuingizwa kwenye kibanda ambapo petroli ilitiririka mpaka kwenye kibanda cha kuchomea viazi (chips). Vibanda zaidi ya 40 vimeteketea kwa moto, tathimini ya mali iliyoteketea bado inafanyika ili kujua thamani halisi ya mali zote zilizoteketea.
Jeshi la polisi mkoa wa mwanza linawataka wananchi kuchukua tahadhari wawapo katika shughuli mbambali kwa kuangalia usalama wao na wawengine.