Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi (Mahakama ya Mafisadi), imewahukumu kifungo cha maisha Mafanyabiashara Abdu Nsembo na Mkewe Shamim Mwacha baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kujihusisha na dawa za Kulevya aina ya Heroin .

Pia mahakama hiyo imetoa amri ya kutaifisha mali za Wahukumiwa ikiwemo gari aina ya Discover 4 ili liwe mali ya Serikali, huku dawa hizo zikitakiwa kuteketezwa.

Hukumu ya kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2020, imetolewa na Jaji Elinaza Luvanda baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kati ya Jamhuri na Utetezi na kujiridhisha kwamba Watuhumiwa wamekutwa na hatia katika makosa mawili ya usafirishaji dawa za Kulevya.

Wawili hao walishtakiwa baada ya kudaiwa Mei Mosi, 2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar  kinyume na sheria ya uhujumu uchumi walikutwa na dawa hizo.