Mkuu wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius Gambosi akimuonyesha jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) mmoja ya mabomu ambayo walikuwa wakiyatumia katia zoezi la utangulizi la kijeshi lililokuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.

 NA TIGANYA VINCENT

VIKUNDI vya watu waliovamia na kubaki katika eneo la Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima lilipo wilayani Kaliua ambao wanaendelea kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji wametakiwa kuondoka kwa hiari kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati wakati akihitimisha zoezi la utangulizi la kijeshi lililo kuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.

Alisema Serikali imeamua kuchukua hatua baada ya kuona kuwa uvamizi katika eneo hilo unaendelea na kutishia uendelevu wa ziwa Tanganyika na kupoteza maisha ya baadhi ya wananchi na watendaji.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema Serikali haiwezi kuendelea kuwacha wavamizi waendelee la uharibifu ambao utaishia ikojia ya eneo hilo ambalo ni muhimu kwa ajili ya upelekaji wa maji ziwa Tanganyika na mapito ya wanyama kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla, Mbuga ya Kigosi Moyosi na Mpanda line.

Alisema Serikali ya Mkoa wa Tabora na Wilaya ya Kaliua wametumia Diplomasia na kutoa elimu ya kutosha kilichobaki watu wote waliomo katika msitu kuondoa wao wenyewe kwa hiari yao.

Dkt. Sengati aliwataka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuhakikisha baada bya kazi iliyofanywa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika eneo wavamizi wasiingie tena na kuharibu maliasi ikiwemo ukataji magogo na uwindaji haramu wa wanyamapori unaofanyika katika eneo hilo.

Aliwataka kufanyakazi kwa kuzingatia maadili na sharia katika kuhakikisha wavamizi wote na vikundi vyote vya uhalifu vilivyomo ndani ya msitu huo vinaondoka ili uharibifu usiendelee.

Alisema lengo la Serikali ni kutaka msitu huo hatimaye uje upande kwa ajili ya kuongeza mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua na Taifa kwa ujumla.

Naye Mkuu wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius Gambosi alisema zoezi hilo ni utangulizi wa zoezi kubwa litakalofanyika katika Hifadhi hiyo limekuwa na mafanikio makubwa ambalo limewaongezea uwezo  na ujuzi wapiganaji.

Alisema kuwa lengo la zoezi hilo ilikuwa ni maandalizi ya zoezi kuwa litakalofanyika katika Hifadhi hiyo hivi karibuni ikiwa ni kuwaweka Makanda kuwa tayari wakati wowote kuliinda Tanzania dhidi ya uchokozi wowote.

Brigedia Jenerali Gambosi alisema zoezi hilo lilinakuja litakuwa la kiwango cha juu.

Aidha alisema kuwa eneo hilo ni muhimu kuhakiisha hakuna wavamizi ndani na kuiomba Serikali kuendelea kutoa elimu kwa watu waliomo ndani yake ili waweze kuondoka kwa hiari kwa ajili ya kulitunza na kuendeleza hifadhi kwa matumizi endelevu ambayo yatakuwa na manufaa kwa wananchi wengi.

Alisema kuendelea kuwaacha wavamizi ndani ya Hifadhi hiyo kunaweza kusababisha hata vikundi vya kiharifu kujificha ndani yake.