Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa matamshi ya Rais wa Marekani Joe Biden kumhusu yanaonyesha matatizo ya zamani na ya sasa yanayoikumba nchi hiyo. 

Putin ameyasema haya alipokuwa akizungumza na wakaazi wa eneo la Crimea katika maadhimisho ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine uliofanyika mwaka 2014. Ameyataja maandamano ya Black Lives Matter kama jambo linaloonyesha kwamba Marekani ina matatizo. 

Msemaji wa rais huyo Dmitry Peskov amesema matamshi hayo ya Biden ni mabaya na yanaonyesha kwamba hataki kurekebisha uhusiano baina ya nchi hiyo mbili. 

Naibu spika wa bunge la Urusi Konstantin Kosachev amesema mbali na kumrudisha nyumbani balozi wa Urusi nchini Marekani, watachukua hatua nyengine ambayo hakuiweka wazi, iwapo Marekani haitoomba msamaha.