Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi amesema Watanzania watafanya kosa kubwa endapo watashindwa kuendeleza yale mema aliyoanzisha na kuyaenzi aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Rais Tshisekedi amesema Dkt. Magufuli amekuwa akitekeleza ndoto zilizokuwa kwa viongozi waasisi wa Bara la Afrika za kuliletea Bara hilo za maendeleo na kupinga vitendo vya ukandamizaji kwa wananchi.

Amesema Dkt. Magufuli ataendelea kukumbukwa na Waafrika wote ambao walimuona kiongozi huyo kama mkombozi wao.

Rais Tshisekedi ameyasema hayo katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma wakati wa shughuli ya kitaifa ya kuaga mwili wa Dkt. Magufuli.