Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi wa Tanzania nchini Japan, Hussein Yahaya Kattanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kushika nafasi ya Dkt. Bashiru Ally ambaye ameteuliwa kuwa Mbunge.

Aidha, Rais Samia ameteua wabunge wapya watatu ambao ni Dkt. Bashiru Ally, Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi Liberata Mulamula.

Rais Samia ametangaza uteuzi huo leo Alhamisi, Machi 31, 2021, mara baada kumaliza kumwapisha Dkt. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbali na uteuzi huo, Rais Samia pia amefanya mabadiliko madogo kwenye Baraza lake la Mawaziri na kusema kuwa walioteuliwa wataapishwa kesho Ijumaa, katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.