Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya baraza la Mawaziri Tanzania

Rais  Samia suluhu Hssan  ametaja mabadiliko hayo mapya ya baraza hilo  jipya la mawaziri wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango.

Mawaziri hao ni  kama ifuatavyo;,Wizara ya Fedha ni Mwigulu Nchemba, ambaye anajaza nafasi ya Makamu wa Rais wa sasa Dkt Philip Mpango.

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, kabla ya uteuzi huu alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, pia amewahi kuhudumu kama Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

Aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Palamagamba Kabudi ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Ofisi ya Rais Tamisemi ameteuliwa Ummy Mwalimu.Ofisi ya rais utumishi na utawala Bora ameteuiliwa Mohamed Mchengerwa.

Zaidi , Tazama Video hapo chini