Rais wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan kesho Jumapili Machi 28,  2021 atapokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za mwaka wa fedha 2019/20.

Pia,  atapokea taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ya mwaka 2019/20.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu,  Gerson Msigwa inaeleza kuwa tukio hilo litarushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio,  televisheni na mitandao kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Hafla ya kupokea taarifa hiyo itafanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.