Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameteua mawaziri watatu huku wawili wakiwa makada wa chama cha ACT-Wazalendo.

Nassor Ahmed Mazrui ambaye ni naibu katibu mkuu wa ACT Zanzibar ameteuliwa kuwa waziri wa afya, ustawi wa jamii, jinsia, wazee na watoto.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Machi 3, 2021 na katibu mkuu kiongozi Zanzibar, Zena Said inaeleza kuwa Omar Said Shaaban ameteuliwa kuwa waziri wa biashara na maendeleo ya viwanda.

Dk Mwinyi pia amemteua Dk Saada Mkuya kuwa waziri wa nchi, ofisi ya makam wa kwanza wa Rais Zanzibar.