Rais wa Malawi,  Lazarus Chakwera amesema kifo cha Rais John Magufuli kimemuumiza kwa kuwa alikuwa mtu muhimu kwake na jina lake linatakiwa kuandikwa kwenye makabati yote barani Afrika na viongozi wafuate mfano mwema wa kiongozi huyo.

Chakwera amesema Afrika itaendelea kumkumbuka zaidi Magufuli kutokana na maamuzi yake mema aliyokuwa akiyafanya kwa maslahi ya watu wake na Afrika.

Akizungumza katika shughuli ya kumuaga Magufuli leo Jumatatu Machi 22, 2021 jijini Dodoma katika uwanja wa Uhuru  amesema, “kulikuwa na maelekezo ambayo yaliacha Afrika ikiwa imeumizwa kwa kiasi kikubwa lakini hawakujua kuwa John Magufuli anakuja, hakika tumempoteza mtu.”

Amemtaja  Magufuli kama mtu aliyekuwa na mapenzi mema na mwanga kwa nchi yake wakati wote na mahali pote alipokuwa.