Mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli utalala Ikulu Zanzibar leo, na kesho asubuhi utasafirishwa kwenda mkoani Mwanza.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, – Kassim Majaliwa katika uwanja wa Amaan jijini Zanzibar, inakofanyika shughuli ya kuaga mwili wa Dkt Magufuli.

Amesema kesho asubuhi mwili Dkt Magufuli utaondoka Zanzibar na kwenda jijini Mwanza ambapo utaagwa na wakazi wa mkoa huo.

Baadaye utasafirishwa kwa gari kwenda wilayani Chato mkoani Geita kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika siku ya Ijumaa, ukipita daraja la Kigongo – Busisi ambapo utasimama kwa muda wa dakika 10 nyumbani kwa mjane wa Dkt. Magufuli, Mama Janeth Magufuli kuwapa nafasi ndugu na jamaa zake kutoa heshima za mwisho.