Aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ataruhusiwa kurudi tena YouTube lakini ni mpaka pale kukiwa na kupungua kwa tishio la kinachodaiwa ni vurugu zinazosababishwa na Wafuasi wake.

YouTube mapema Mwezi January mwaka huu iliifuta akaunti ya Trump kama ilivyofanya mitandao mingine ikiwemo Facebook na Twitter kwa madai ya kwamba zilitumika kuchochea vurugu kwenye majengo ya Bunge.

“Tutamruhusu Trump kurejea YouTube kama matishio yatapungua, Polisi wamesema kuna wasiwasi wa majengo ya Bunge kuvamiwa tena, ni wazi bado tatizo lipo”- Susan, Wojcicki, Boss wa YouTube