Joan Laporta (58) amechaguliwa kuwa Rais mpya wa FC Barcelona baada ya kupata ushindi wa asilimia 54 ya kura zote zilizopigwa.

Laporta aliyewahi kuwa Rais wa FC Barcelona kwa miaka 7 (2003-2010) na kumuibua Lionel Messi na kumuamini Pep Guardiola, aliahidi kuwa akishinda Urais atahakikisha Messi haondoki Barcelona.


Joan Laporta anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Josep Maria Bartomeu aliyejiuzulu October 2020, katika utawala wake wa mwanzo Laporta aliwasajili Ronaldinho na Samuel Eto’o usajili ambao ulizaa matunda na kushinda Ligi ya Mabingwa mara mbili, LaLiga mara 4 na Copa der Rey.