Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa kurefusha hatua za karantini hadi mwezi ujao wa Aprili wakati nchi hiyo ikiwa inapambana na wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona. 

Vizuizi vya sasa vya kukabiliana na kuongezeka kwa maambukizi vinamalizika mwishoni mwa mwezi huu wa Machi. 

Kwa mujibu wa taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza nchini Ujerumani, Robert Koch idadi ya maambukizi mapya kwa alama 100 kwa kila wakaazi 100,000 kote nchini imeongezeka ndani ya siku chache zilizopita. 

Kansela Merkel na viongozi wa majimbo yote 16 ya Ujerumani watayajadili hayo kwenye mkutano wa siku ya leo Jumatatu. 

Merkel amewataka Wajerumani kuwajibika zaidi wakati wa janga hili na kuacha kusafiri kwenda kwenye kisiwa maarufu cha Uhispania cha Mallorca wakati wa mapumziko ya Pasaka