Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price amesema jana kuwa kundi la waasi wa Houthi nchini Yemen lazima lionyeshe kujitolea kwake kushiriki katika mchakato wa kisiasa wa kuafikia amani nchini Yemen baada ya kundi hilo kudai kuhusika katika mashambulio ya ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya Saudi Arabia.

Price ameongeza kuwa viongozi wa kundi hilo la waasi lenye mafungamnao na Iran wanapaswa kukomesha mashambulio na kujihusisha na mazungumzo, hii ikiwa njia ya pekee ya kupata ufanisi kwa sulushisho la kisiasa linalotafutwa. 

Viongozi wa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia wamesema kuwa ndege nyingi zisizo na rubani na makombora zilinaswa kabla ya kufikia malengo yake na kwamba hakuna waathiriwa wala uharibifu wa mali uliosababishwa na mashambulio hayo.

Price amesema mashambulio hayo hayakubaliki na kwamba yanahatarisha maisha ya raia wanaowajumuisha wale wanaotoka Marekani.

-DW