Wanajeshi wa DRC Wakiwa katika Dorian

Marekani inasema makundi ya waasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na nchini Msumbiji ni magaidi kutoka nje ya nchi hiyo.

Nchini DRC, kundi la ADF limetajwa kuwa la kigaidi huku Al Ansar al-Sunna, linalofahamika kama Al-Shabaab nchini Msumbiji, yakitajwa kushirikiana na kundi la kijihadi la Islamic State.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani imesema viongozi wa makundi hayo, wanashirikiana kwa karibu na wale wa Islamic State na sasa wamekewa vikwazo.

Kundi la ADF limeendelea kusababisha ukosefu wa usalama Mashariki mwa DRC hasa katika Wilaya ya Beni na tangu kuanza kwa mwaka 2021, limesababisha vifo vya mamia ya raia.

Nalo kundi la Ansar al-Sunna, limetekeleza mauaji ya zaidi ya watu 1,300 nchini Msumbiji tangu Oktoba mwaka 2017.