Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amempongeza rais mpya wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, na kusema kuwa Marekani iko tayari kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili. 

Harris, mwanamke wa kwanza na mtu wa kwanza wa rangi kushika wadhifa wa Makamu wa Rais Marekani alituma pongezi zake kwa Suluhu kupitia mtandao wa Twitter. 

Ofisi ya Mwakilishi wa Biashara ya Marekani inaongoza juhudi za kujenga ushirika mpya wa kibiashara na uwekezaji na Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha mataifa ya Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.