Mwili wa ailiyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli umewasili jijini Mwanza ili kutoa nafasi kwa wakazi wa jiji hilo na viunga vya jirani kutoa heshima zao za mwisho kwa mpendwa wao.

Katika uwanja wa ndege wa Mwanza mwili wa Dkt. Magufuli umepokelewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa na viongozi wengine wa mkoa wa Mwanza.

Mara baada ya kuwasili mwili huo unapitishwa katika barabara ya Airport na kuelekea Nyamanoro, Pasiansi, Kiloleni, Montessori, Maduka 9, Nyasaka, Buzuruga, Mabatini, Mlango Mmoja, Nata, Mnara wa Nyerere, Mjini kati kuelekea CCM Kirumba.

Mwili huo umesimama kwa Dakika moja katika eneo la Selemani Nassoro ikiwa ni kutoa heshima katika eneo hilo ambalo Dkt. Magufuli aliishi kipindi cha nyuma akiwa jijini Mwanza.

Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza wamejipanga katika barabara hizo huku wakiimba “Magufuli Jeshi” na wengine kuangua vilio kutokana na kuzidiwa na huzuni baada ya kuondokewa na mpendwa wao.