Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mafinga kinatarajia kuongeza  uzalishaji maziwa kutoka Lita 250 hadi 1,000 kwa siku ili kukikidhi mahitaji ya vikosi vya Jeshi hilo, ikiwemo kuuza katika soko la ndani.

Aidha amesema Jeshi limejipanga kuongeza idadi ya ng’ombe wa nyama na maziwa wanaofugwa katika kambi ya Jeshi hilo, lengo ikiwa ni kutekeleza agizo la Mkuu wa Jeshi hilo la kuwataka kujitegemea katika mahitaji ya chakula badala ya kusubiri fedha za serikali.

Kaimu Kamanda wa Kikosi 841 Mafinga JKT, Luteni Kanali Issa Chalamila amesema hivi sasa kikosi hicho kinazalisha lita 250 za maziwa kwa siku,lakini  mikakati walioiweka ni kufikia kuzalisha lita 1,000 kwa siku.