Mwaka mmoja baada ya mauaji ya Mmarekani mweusi George Flloyd, kesi ya mmoja ya polisi wa zamani aliyehusika na kifo chake imeanza siku ya jana. 

Derek Chauvin mshitakiwa mkuu katika kesi hiyo anakabiliwa na kosa la mauaji na huenda akahukumiwa miaka 40 jela katika jimbo la Minnesota iwapo atapatikana na hatia. 

Kesi hiyo inayofanyika katika jimbo la Minneapolis inaaza hii leo kwa kuwachagua majaji watakaoisimamia huku mchakato kamili wa kesi hiyo ukitarajiwa kuanza tarehe 29 mwezi Machi. 

Kifo cha George Floyd mwanamme mweusi aliyekuwa bila silaha kilisababisha maandamano makubwa dhidi ya unyanyasaji unaofanywa na polisi pamoja na ubaguzi wa rangi nchini Marekani. 

Watu wengi pia walindanamana katika mataifa mengine duniani katika maandamano yaliopewa jina la Black Lives Matter-Maisha ya mtu mweusi yana thamani.