Kamati ya Kudumu ya bunge ya sheria ndogo imekutana na Viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiongozwa na Waziri Mhe. Innocent Bashungwa. Kamati hiyo ilikutana kujadili kuhusu Kanuni za Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 1976 pamoja na maendeleo ya tasnia hiyo,

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Ridhiwani Kikwete Mbunge wa Chalinze, imejadili juu ya sheria zilizopo na na jinsi ya kuziboresha ili kuweka mazingira rafiki kwa wadau wa tasnia ya Filamu nchini na kwenda sambamba na kasi ya kiteknolojia inayokuwa kila siku hasa katika usajili na uhakiki wa kazi zao.

Kikao hicho kimekaliwa  tarehe 29 Machi, 2021 Jijini Dodoma. Hata hivyo, katika kuunga mkono juhudi za Kamati hiyo ya Bunge, Serikali ilikuwa katika hatua ya kukusanya maoni ya wadau juu ya maeneo gani kwenye Kanuni za Filamu na Michezo ya Kuigiza yaboreshwe.