Ikulu ya Marekani imeliomba Shirika la Afya Duniani (WHO) kuanza awamu nyingine ya ufuatiliaji ili kujua kiini cha Corona baada ya WHO kusema wameshindwa kubaini chanzo hasa cha Corona licha ya kufanya uchunguzi wa kutosha wakiwa na Timu ya Wataalamu.

Marekani bado inaamini Corona ni virusi vilivyozalishwa maabara China na kusema China haikutoa Ushirikiano kwa Wataalamu na inaficha taaarifa muhimu lakini China bado inakana tuhuma hizo.