Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera
Halmashasuri Ya Wilaya Ya Missenyi Mkoani Kagera Inatarajia Kuajili Watumishi 1,075 Katika Idara Mbalimbali,  watumishi  918 wanatarajia kupandishwa madaraja na watumishi zaidi ya 180 wanatarajia kubadilishiwa muundo katika  idara mbalimbali wilayani humo kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022

Hayo yalibainishwa na afisa mipango wa wilaya hiyo bw.Juliani  Talimo wakati akisoma taarifa ya bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022  march 10 katika kikao maalumu cha baraza la madiwani la  halmashauri hiyo wakati wakijadili na kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022.


Kwa mwaka wa fedha2021/22 jumla ya  billion 51,485,581,187 ndizo zimekadiliwa kutumika katika kukidhi mahitaji ya halmashauri hiyo ili kutimiza majukumu mbalimbali.


Kwa mujibu wa taarifa  iliyosomwa  katika kikao hicho zaidi ya billion 3.6 zinatathiminiwa kukusanywa kutoka katika mapato ya ndani ya hamashauri hiyo.


Nao madiwani mbalimbali  walipata nafasi ya kuzungumzia  bajeti iliyowasilishwa akiwemo diwani wa kata ya Gera bw. Henery Bitegeko na kueleza kuwa bajeti wameipokea na kushukuru menejimenti ya halmashauli hiyo chini ya mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo Innocent Mukandala.


Naye mwenyekiti wa halmashauri hiyo bw. Projestus Tegamaisho aliwataka waandaaji wa makablasha kuhakikisha wanakamilisha taarifa kwa muda bila kuacha mashaka na katika kikao hicho ametilia mashaka taarifa ya miradi katika upande wa elimu.