Katika ushindani wa soko la simu kampuni nyingi za simu zimejikuta zikitoa simu zenye kushabihiana sifa. Kwa leo tuliangalizie kwa ndani simu aina ya
Infnix Hot 10 Play na Samsung Galaxy A02s.na mwisho wa makali hii nadhani tutakuwa tumepata kufahamu ipi ni simu sahihi kwako kotokana na matumizi yako.

Sifa za Ndani (CPU, Chipset, RAM na ROM)

Kwa upande wa sifa za ndani, Infinix Hot 10 Play inakuja na CPU yenye uwezo zaidi hadi Octa-core (2x2.0 GHz Cortex-A75 & 6x1.8 GHz Cortex-A55), huku Galaxy A02s ikiwa nyuma yake kwa kuwa na CPU yenye uwezo wa hadi Octa-core 1.8 GHz Cortex-A53.

Mbali na hayo, Infinix Hot 10 Play inakuja na Chipset ya MediaTek Helio G35, wakati Galaxy A02s inakuja na Chipset ya Qualcomm Snapdragon 450. Chipset zote zinakuja na uwezo tofauti n ani rafiki hata katika uchezaji games kupitia simu hizo.

Kwa upande mwingine wa RAM, Infinix Hot 10 Play inakuja na RAM ya GB 4, huku Galaxy A02s yenyewe ikiwa inakuja na RAM kati ya GB 3. Tukiangalia uhifadhi wa ndani, Galaxy A02s inakuja na ROM ya GB 32, huku pia Infinix Hot 10 Play nayo inakuja na ROM ya hadi GB 64.

Uwezo wa Battery

Infinix Hote 10 Play ni moja kati ya simu ambayo ipo kwenye list ya simu zinazodumu na chaji zaidi mwaka 2021, hii ni kwa sababu simu hii inakuja na battery kubwa yenye uwezo wa hadi 6000 mAh, huku ikiwezeshwa na teknolojia ya kufanya ijae na chaji kwa haraka yaani Fast charging yenye uwezo wa 10 Wh. Galaxy A02s yenyewe inakuja na battery ya 5000 mAh, huku nayo ikiwa na Fast charging ya hadi 18 Wh.

Muundo

Kwa kuanza, tuakiangalia muundo wa simu zote mbili, zote zimetengenezwa kwa plastiki, hii ikiwa na maana muundo wa nyuma wa simu hizi ni plastiki, na hata fremu yake pia ni plastiki. Kwa nyuma Infinix Hot 10 Play inakuja na sehemu ya ulinzi ya fingerprint, huku Galaxy A02s yenyewe ikiwa haina sehemu hiyo kabisa.

Kioo

Kwa upande wa kioo Infinix hot 10 play inakuja na kioo kikubwa wa inch 6.82, huku Galaxy A02s ikiwa inakuja na kioo cha inch 6.5. Mbali na hayo, kioo cha Infinix Hot 10 Play kimetengezwa kwa teknolojia ya IPS LCD, wakati kioo cha Galaxy A02s kikiwa kimetengezwa kwa TFT/PLS IPS. Kwa upande wa resolution simu zote mbili zinakuja na uwezo wa 720p.

Kamera

Kwa upande wa kamera Samsung Galaxy A02s na Infinix Hot 10 Play zote zinakuja na kamera kuu za nyuma za Megapixel 13, huku Galaxy A02s ikiwa na kamera mbili zaidi zenye Megapixel 2 kila moja. Hii inafanya simu ya Galaxy A02s kuwa na Kamera tatu, huku Inifnix Hot 10 Play ikiwa na kamera mbili kwa nyuma.

Kwa upande wa kamera za mbele, Infinix Hot 10 Play inakuja na kamera ya Megapixel 8, huku Galaxy A02s ikiwa inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 5. Pia kamera hiyo ya Infinix Hot 10 Play inakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps. Vilevile Infinix Hot 10 Play inakuja na LED flash kwenye kamera ya mbele, wakati Galaxy A02s yenyewe haina sehemu hiyo.

Mfumo wa Undeshaji

Kwa upande wa mfumo wa uendeshaji, Galaxy A02s inakuja na mfumo wa uendeshaji wa Android 10, huku Inifnix Hot 10 Play nayo pia ikija na mfumo wa Android 10 ambao ni Go Edition. Simu ya infinix inakuja na mfumo mpya wa XOS 7, wakati Galaxy A02s ikiwa inakuja na mfumo wa One UI.

Uwezo wa Battery

Infinix Hote 10 Play ni moja kati ya simu ambayo ipo kwenye list ya simu zinazodumu na chaji zaidi mwaka 2021, hii ni kwa sababu simu hii inakuja na battery kubwa yenye uwezo wa hadi 6000 mAh, huku ikiwezeshwa na teknolojia ya kufanya ijae na chaji kwa haraka yaani Fast charging yenye uwezo wa 10 Wh. Galaxy A02s yenyewe inakuja na battery ya 5000 mAh, huku nayo ikiwa na Fast charging ya hadi 18 Wh.

Bei za Makadirio

Kwa upande wa Bei, Inifnix Hot 10 Play inapatikana kwa bei ya makadirio kuanzia TZS 350,000 wakati Galaxy A02s inapatikana kwa bei ya makadirio kuanzia TZS 450,000. Kumbuka bei hizi ni makadirio na zinaweza kubadilika kulingana na eneo unalo nunua simu hizi.

Upatikanaji

Kwa sasa simu zote zinapatikana hapa Tanzania, huku Infinix Hot 10 Play ikiwa inapatikana kupitia kwenye maduka ya kampuni ya kutoa huduma za simu ya Tigo Tanzania, pamoja na maduka ya simu ya Infinix kote Tanzania ikiwa na ofa ya GB 18