Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais.


Jina la Mpango limesomwa bungeni mjini Dodoma leo Jumanne Machi 30, 2021 na Spika Job Ndugai aliyeletewa bahasha yenye jina hilo na mpambe wa kiongozi mkuu huyo wa nchi.

Jina la Dk Mpango liliwekwa katika bahasha mbili ya juu ilikuwa ya kaki na ya ndani ilikuwa nyeupe, Spika Ndugai alianza kusoma nyaraka hiyo ya rais akirudia rudia maneno ya utangulizi kabla ya kulisoma jina.

Baada ya kusoma jina wabunge walishangilia kwa nguvu  huku Dk Mpango akionekana kushikwa na butwaa huku  wabunge wakinyanyuka kwenye viti vyao na kumfuata kumpongeza..