Mwanasiasa wa upinzani na aliyekuwa mgombea urais Robert Kyagulanyi, anayefahamika kwa jina maarufu Bobi Wine, amekamatwa jijini Kampala.


Wakati anakamatwa alikuwa ameongozana na timu ya wabunge wa chama chake katika maandamano kupinga kukamatwa na kutoweka kwa wafuasi wa chama hicho wakati na baada ya uchaguzi huo.

Vikosi vya usalama vilifyatua mabomu ya machozi kutawanya waandamaji waliokuwa wameandamana na mwanasiasa huyo.

Habari zinaeleza kuwa mbali na Bobi, wabunge 15 wa chama hicho wamekamatwa.