Mama Sarah Obama ambaye ni bibi wa Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, amefariki dunia, familia imethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Mama Sarah alikuwa akiugua kwa muda mrefu na amefariki wakati akipatiwa matibabu katika hospitali moja iliyopo katika Mji wa Kisumu nchini Kenya.

Marehemu alikuwa mke wa tatu wa Hussein Obama, amefariki akiwa na umri wa miaka 99 na anatarajiwa kuzikwa leo kwa mujibu wa taratibu na sheria ya dini ya kiislamu.

Obama ambaye ni mjukuu wa Mama Sarah aliwahi kuwa Rais wa 44 wa Marekani akiwa ni mwenye asili ya Afrika kutokea nchini Kenya.