Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewasihi na kuwasisitiza zaidi wananchi kuzingatia tahadhari zote ikiwemo uvaaji wa barakoa

Taarifa hiyo iliyotolewa  Jumapili, Februari 21, 2020 na Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano kwa umma, Gerard Chami alisema wizara inaendelea kusimamia na kusisitiza utekelezaji wa tahadhari ya magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza na ya kuambukiza yakiwemo ya milipuko ikiwemo tishio la ugonjwa wa COVID-19.

Alitaja tahadhari zingine ikiwemo kunawa mikono, kutumia vipukusi (sanitizer),  kufanya mazoezi a, kuwalinda wale wote walio katika hatari kama wazee, watu wanene, na wenye magonjwa ya muda mrefu.

Kupata lishe bora ikiwemo matunda na mbogamboga, matumizi ya tiba asili zilizosajiliwa na baraza la tiba asili na kama inavyoelimishwa na wataalamu husika na kuwahi katika vituo vya kutolea huduma za afya mara uonapo dalili za maradhi ili watoa huduma wapate nafasi nzuri zaidi ya kutibu.