Timu ya shirika la afya duniani, WHO, iliyokwenda Wuhan imesema virusi vya Corona huenda havikuanzia katika maabara ya China na kuna uwezekano mkubwa kwamba virusi hivyo viliingia kwa binadamu kutoka kwa mnyama.

 Hayo yameelezwa na mtaalamu wa timu hiyo wakati ujumbe huo wa WHO ukikamilisha ziara yake ya kutafuta vilipoanzia virusi hivyo. 

Wataalamu wa shirika hilo la WHO waliofanya ziara Wuhan wanaziangalia njia nyingi, kutafakari ni kwa jinsi gani virusi hivyo vilimfikia binadamu na kusababisha janga kubwa ambalo kufikia sasa limewauwa zaidi ya watu milioni 2.3 duniani kote.

Taasisi inayohusika na virusi ya Wuhan nchini China ilikusanya sampuli chungunzima hatua ambayo ilizusha tuhuma kwamba huenda ilikuwa chanzo cha mripuko huo, japokuwa China inayapinga vikali madai hayo.